Entertainment

Chief God Love Asema “Chakacha” ya Pipi Jojo Italeta Grammy Afrika Mashariki

Chief God Love Asema “Chakacha” ya Pipi Jojo Italeta Grammy Afrika Mashariki

Meneja wa muziki Chief God Love amedai hakuna msanii wa filamu au muziki nchini Tanzania ambaye amewahi kutoa video kali kama ya wimbo wa msanii wake uitwao “Chakacha” inayotarajiwa kutoka mwezi Novemba.

God Love amesema kuwa video hiyo itakuwa ya kipekee barani Afrika na kwamba itainua hadhi ya muziki wa Afrika Mashariki hadi ngazi za kimataifa. Anaamini kazi hiyo itafungua milango ya tuzo kubwa kama Grammy kwa wasanii wa eneo hilo.

Aidha, amewaonya wasanii wanaopanga kuachia video zao mapema mwezi Novemba kuzingatia ratiba zao, akisisitiza kuwa wimbi la Chakacha litatawala anga za muziki na kuzima juhudi za wengine kupata umaarufu.

Video ya Chakacha, inayotoka kwa msanii Pipi JoJoh, inatarajiwa kuachiliwa rasmi mwezi Novemba, huku mashabiki wakisubiri kwa hamu kuona ubunifu na ubora uliotajwa na meneja huyo anajiita billionea.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *