LifeStyle

Mtangazaji wa Kenya Ajitetea Kuhusu Nyumba ya Elfu 55

Mtangazaji wa Kenya Ajitetea Kuhusu Nyumba ya Elfu 55

Mtangazaji wa radio nchini Kenya, Kamene Goro amejitetea vikali mitandaoni baada ya kuzushiwa kwamba anadanganya kuhusu kodi ya nyumba ya shillingi 55,000 aliyokuwa analipa kipindi anajitafuta kimaisha.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Kamene amesema kuwa kila mtu ana mwanzo wake tofauti maishani, na watu hawapaswi kulinganisha safari zao na za wengine, akisisitiza kuwa wale wanaofahamu maisha yake halisi wataelewa zaidi anachomaanisha.

Kauli yake imekuja kufuatia mjadala uliotanda mitandaoni baada ya kusema kuwa alipokuwa akiianza maisha mjini, aliwahi kuishi kwenye nyumba ya bei rahisi yenye kodi ya shilingi elfu 55 kwa mwezi.

Wengi walidai kuwa kiasi hicho hakiwezi kuelezwa kama bei rahisi kwa mtu anayeanza maisha, jambo lililosababisha ukosoaji mkubwa. Baadhi ya wafuasi wake hata hivyo walimtetea wakisema huenda alizungumza kulingana na hali yake ya kifedha kwa wakati huo, na kwamba kauli yake haikupaswa kutafsiriwa vibaya.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *