Gossip

Phoina Akanusha Kuwa Katika Mahusiano na Khalif Kairo

Phoina Akanusha Kuwa Katika Mahusiano na Khalif Kairo

Mjasiriamali maarufu wa urembo, Phoina, ameibuka na kukanusha madai kwamba yuko kwenye uhusiano wa kimapenzi na mfanyabiashara wa magari Khalif Kairo, baada ya video yao kusambaa mtandaoni ikionyesha wakipigana mabusu hadharani.

Video hiyo, ambayo imezua gumzo kubwa mitandaoni, ilionekana kuonyesha ukaribu wa wawili hao, hatua iliyowafanya mashabiki na watumiaji wa mitandao ya kijamii kuanza kukisia kuwa huenda wanadate.

Hata hivyo, katika mahojiano na Mwende Macharia, Phoina amefafanua kuwa tukio hilo halikuwa la kimapenzi na lilitafsiriwa vibaya na umma. Ameweka wazi kuwa kilichoonekana kwenye video kilikuwa sehemu ya burudani tu, akisisitiza kuwa hana uhusiano wowote wa kimapenzi na Kairo.

Phoina ameendelea kuwaomba mashabiki kutotengeneza hadithi zisizo na msingi kuhusu maisha yake ya kibinafsi, na kuelekeza nguvu zao zaidi katika kuunga mkono kazi na biashara zake.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *