LifeStyle

Huddah Monroe Akosoa Kampuni za Ulinzi Kenya

Huddah Monroe Akosoa Kampuni za Ulinzi Kenya

Mjasiriamali na mshawishi wa mitandaoni, Huddah Monroe, ameibua mjadala mkali mitandaoni baada ya kukosoa kampuni za ulinzi nchini Kenya kwa kuendelea kuwapa wanawake, wakiwemo single mothers, zamu za usiku.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Huddah ametaja kuwa ni jambo lisilo la kawaida kwa wanawake kupewa zamu za usiku wakati wanahitajika zaidi nyumbani kwa ajili ya watoto wao.

Huddah amesema kuwa watoto, hasa wa umri mdogo, wanahitaji uwepo na uangalizi wa mama zao wakati wa usiku kwa sababu ndiyo muda ambao wengi wanapata usalama wa kihisia, mwongozo na utulivu.

Ameongeza kuwa kampuni zinazotoa ratiba hizo hazizingatii changamoto za single mothers, ambao mara nyingi hawana mtu wa kubadilishana majukumu nao nyumbani.

Mrembo huyo hata hivyo ametoa changamoto kwa kampuni za ulinzi nchini Kenya kuunda mwongozo utakaowaruhusu wanawake kupata mapumziko wakati wa usiku, kwani ratiba za kazi za usiku huathiri ustawi wa familia.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *