Entertainment

Dulla Makabila Atoa  Milioni 120 Taslimu  Kusaidia Wasanii wa Singeli

Dulla Makabila Atoa  Milioni 120 Taslimu  Kusaidia Wasanii wa Singeli

Staa wa muziki wa Singeli, Dulla Makabila, ameibua gumzo mtandaoni baada ya kuonekana akiwa na kifurushi cha pesa kinachokadiriwa kufikia Tsh milioni 120, akidai kuwa kiasi hicho kimetengwa mahsusi kwa ajili ya kusaidia wasanii wenzake wa Singeli ili waendelee kusimama imara kwenye game.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Dulla Makabila amechapisha video akionesha fedha hizo huku akiwataka mashabiki kuwataja wasanii wa Singeli wanaohitaji mtaji au uwekezaji ili kuendeleza kazi zao. Amesema lengo lake ni kuinua vipaji na kuhakikisha muziki wa Singeli unaendelea kukua bila wasanii wengi kukata tamaa kutokana na changamoto za kifedha.

Dulla pia ametumia nafasi hiyo kuwashukuru wasanii Mbosso na Bien kwa kazi yao ya Power Remix, akisema wimbo huo umekuwa miongoni mwa nyimbo zilizompa motisha na kumchangamsha katika kipindi anachohesabu fedha na kupanga mipango yake ya uwekezaji.

Hatua yake imepongezwa na mashabiki na wadau wa muziki, hasa ikizingatiwa kwamba Singeli imekuwa ikikua kwa kasi lakini wasanii wengi bado hukumbana na changamoto za rasilimali. Mashabiki wanatarajia kuona utekelezaji wa ahadi hiyo na namna itakavyobadili maisha ya wasanii wanaochipukia katika miondoko hiyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *