Entertainment

Iyanii Ashinda Tuzo Mbili Kubwa

Iyanii Ashinda Tuzo Mbili Kubwa

Msanii nyota wa Afropop, Iyanii, ameendelea kung’ara kwenye tasnia ya muziki baada ya kushinda tuzo mbili katika hafla ya utoaji tuzo za Jamhuri mwaka huu Jijini Nairobi.

Iyanii ametia kibindoni tuzo ya Best Male Artist of the Year, kutokana na mchango wake mkubwa na kazi zilizotamba nchini Kenya. Lakini pia ameshinda tuzo ya Music Collaboration of the Year kupitia single yake Donjo Maber, kazi iliyopokelewa kwa ukubwa na mashabiki.

Kupitia Instastory yake, Iyanii amewashukuru mashabiki wake kwa kuamini safari yake ya muziki na kueleza kuwa ushindi huo ni hatua nyingine muhimu katika historia yao ya pamoja.

Iyanii ambaye kwa muda amekuwa na njaa ya mafanikio, ameongeza kuwa kilicho mbele sasa ni malengo makubwa zaidi, ikiwemo kutazamia tuzo za kimataifa kama Grammy.

Ushindi huu unathibitisha nafasi ya Iyanii kama mmoja wa wasanii wanaoendelea kuipa sura mpya muziki wa kizazi kipya nchini Kenya

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *