Sports news

Lukenya University Yapanga Mbio Kubwa Zaidi 2026

Lukenya University Yapanga Mbio Kubwa Zaidi 2026

Mbio za marathoni za Lukenya University Ten Million Trees zimeratibiwa kurejelewa mwaka ujao, huku waandalizi wakithibitisha kuwa makala ya nne yataandaliwa tarehe 28 mwezi Machi mwaka 2026, mjini Mtitu Andei.

Kulingana na waandalizi mbio hizo zinatarajiwa kuwa kubwa zaidi huku mashindano hayo yakishirikisha mbio za wanariadha wenye uzoefu na washiriki wengine. Kilele cha mashindano hayo ni mbio za kilomita 42, ambapo wanariadha wenye uzoefu watapigania zawadi ya shilingi laki tano. Mbio hizo zitashirikisha vitengo viwili, wanaume na wanawake.

Mashidnado hayo pia yatashirikisha mbio za kilomita 21, mbio za kilomita 10, mbio za kilomita 5, na mbio za Black Mamba za kilomita 21 ambazo zitashirikisha wakazi wa Kibwezi Mashariki.  Kwa wapenda baiskeli, waandalizi wameanzisha mbio maarufu za baiskeli za milimani za kilomita 42, zilizoundwa kwa ajili ya waendeshaji walio tayari kushindana katika maeneo magumu.

Mashindano hayo yanaendelea kutetea uendelevu wa mazingira, huku maelfu ya miti yakitarajiwa kupandwa kama sehemu ya mpango wa upanzi wa Miti Milioni Kumi. Chuo Kikuu cha Lukenya kimesema kuwa maandalizi yanaendelea kwa njia mwafaka, na makala ya mwaka huu yanatarajiwa kuvutia idadi kubwa ya washiriki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *