Msanii nyota kutoka nchini Uganda, Sheebah Karungi, anatuhumiwa kuvunja ndoa ya promota wa muziki anayeishi London, Jaffer, baada ya madai kuibuka kwamba wawili hao wanadaiwa kupata mtoto wa kiume pamoja.
Kwa mujibu wa chanzo cha karibu na familia ya promota huyo, Jaffer alithibitisha hadharani kuwa yeye ndiye baba wa mtoto wa Sheebah, tamko ambalo lilitikisa ndoa yake na mke wake wa kwanza, Diana, na kusababisha mgawanyiko mkubwa katika familia yao.
Chanzo hicho kimeeleza kuwa Diana aliamua kuondoka kwenye ndoa mara tu alipopata uthibitisho wa ujauzito wa Sheebah. Inadaiwa kuwa alisitisha kabisa mawasiliano na Jaffer kutokana na mshtuko na maumivu ya usaliti huo.
Taarifa za ndani zinaarifu kuwa kabla ya sakata hilo kuibuka, Sheebah na Diana walikuwa marafiki wa karibu. Hata hivyo, urafiki wao unadaiwa kuvunjika baada ya Sheebah kuanzisha uhusiano wa siri na Jaffer. Vyanzo vimedokeza pia kuwa msanii King Saha anatajwa kuhusika katika kuwaunganisha wawili hao.
Kwa sasa, taarifa zinaeleza kuwa Sheebah ndiye yuko katika mahusiano na Jaffer, hatua ambayo inatajwa kuchangia kuvunjika kwa ndoa ya promota huyo na mke wake wa kwanza, Diana.