Msanii wa vichekesho na mwanaharakati wa kijamii, Eric Omondi, ametoa wito kwa wasanii nchini Tanzania kuungana kupinga udhalimu na kutokubali kutumika kisiasa kwa njia zinazoharibu taswira na brand zao.
Akipiga stori na Plug TV, Omondi amesema kuwa muziki na sanaa kwa ujumla hubaki mioyoni mwa watu kwa muda mrefu zaidi kuliko siasa, akisisitiza kuwa wasanii wanapaswa kulinda heshima na ushawishi wao kwa jamii.
Kwa mujibu wake, kujihusisha na siasa za upande mmoja kunahatarisha uaminifu wa wasanii kwa mashabiki wao, na badala yake wanapaswa kutumia majukwaa yao kuhamasisha haki, umoja na mabadiliko katika jamii.
Kauli yake imekuja baada ya baadhi ya wasanii nchini Tanzania kuunga mkono serikali iliyochaguliwa katika uchaguzi wa Oktoba 28, uchaguzi ambao ulizua utata na kupingwa na wananchi waliodai haukuwa huru na wa haki.