Gossip

Ndugu wa Gloria Ntazola Aomba Radhi Hadharani Baada ya Sakata la Familia

Ndugu wa Gloria Ntazola Aomba Radhi Hadharani Baada ya Sakata la Familia

Ndugu wa Socialite Gloria Ntazola ameomba radhi hadharani kufuatia sakata lililozua taharuki katika familia yao.

Akipiga stori na mwanamitandao aitwaye 2Mbili, kijana huyo amekiri kusumbua familia na kuleta hali ya sintofahamu. Ameeleza kuwa anatamani kufunguliwa biashara ili kuanza upya na kujitegemea, akisisitiza kuwa hatua hiyo itamsaidia kurejesha imani ya familia na jamii.

Kauli yake imekuja mara baada ya Gloria Ntazola kumfukuza kijana huyo nyumbani kwake kufuatia madai ya kumpiga mama yao mzazi na matumizi ya dawa za kulevya, jambo lililosababisha mzozo mkubwa wa kifamilia.

Sakata hili linaendelea kuvutia hisia za mashabiki na wadau wa kijamii, huku wengi wakisubiri kuona kama familia ya Ntazola itakubali ombi hilo na kumsaidia kuanza upya.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *