Msanii wa Bongo Fleva Rayvanny na nyota wa kimataifa Nora Fatehi wamewafikia mashabiki wao kwa ujumbe wa shukrani baada ya ushindi mkubwa kwenye EAEA Awards, ambako wimbo wao “Oh Mama Tetema” umeibuka mshindi wa Video Bora ya Mwaka.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Rayvanny amepakia video ya Nora Fatehi akitoa shukurani kwa mashabiki wote waliounga mkono kazi hiyo. Katika video hiyo, Nora amewashukuru kwa upendo na sapoti waliyoonyesha tangu kutolewa kwa wimbo huo ambao umeendelea kufanya vizuri kimataifa.
Mbali na ushindi wa “Oh Mama Tetema”, Nora Fatehi pia aliibuka kidedea kwa kutwaa tuzo ya Best Video kupitia wimbo wake “Snakes” aliomshirikisha staa wa Marekani, Jason Derulo.
Tuzo hizo mbili zimeongeza uthibitisho wa nafasi yake kama mmoja wa wasanii wa kimataifa wanaoendelea kutamba kwa mafanikio makubwa kwenye muziki na video.