Entertainment

Nadia Mukami Akanusha Kuiba Ubunifu wa Zuchu na Kutumia Kwenye Wimbo Wake Mpya

Nadia Mukami Akanusha Kuiba Ubunifu wa Zuchu na Kutumia Kwenye Wimbo Wake Mpya

Msanii wa muziki kutoka Kenya, Nadia Mukami, ameweka wazi msimamo wake kufuatia madai yaliyosambaa mitandaoni kwamba wimbo wake mpya Woza ulinakiliwa au kusampuliwa kutoka kwa msanii wa Tanzania, Zuchu.

Akizungumza kuhusu suala hilo, Nadia amesisitiza kuwa Woza haujanakiliwa wala kusampuliwa kutoka kwa wimbo wowote wa Zuchu. Ameeleza kuwa kilichofanyika ni yeye na mtayarishaji wake, Teknixx, kuamua kutumia mtindo wa sauti unao-trend kwa sasa katika ukanda wa Afrika Mashariki.

Kwa mujibu wa Nadia, mdundo huo si mali ya msanii mmoja bali ni mtindo wa muziki unaotumiwa na wasanii wengi wa kikanda wanaotaka kwenda na mwelekeo wa soko la sasa. Ameongeza kuwa wasanii wengi kutoka nchi mbalimbali wamekuwa wakitumia aina hiyo ya sauti bila kuhusishwa na wizi wa kazi za wengine.

Msanii huyo amesisitiza kuwa ubunifu katika muziki hubadilika kulingana na wakati, na ni jambo la kawaida kwa wasanii kukumbatia mitindo mipya ili kubaki relevant katika tasnia inayobadilika kwa kasi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *