Gossip

Huddah Monroe Asema Alitabiri Mapema Rais Ruto Atakuwa Rais wa Kenya

Huddah Monroe Asema Alitabiri Mapema Rais Ruto Atakuwa Rais wa Kenya

Socialite maarufu nchini Kenya, Huddah Monroe, amesema alitabiri mapema kuwa William Ruto angekuwa Rais wa Kenya siku moja, hata kabla hajaimarika kisiasa.

Kupitia InstaStory, Huddah amechapisha picha ya zamani akionekana akiwa pamoja na Rais Ruto kipindi ambacho alikuwa bado anajitafuta na kujijenga katika ulingo wa siasa za kitaifa. Sambamba na picha hiyo, Huddah amesema aliwahi kumwambia rafiki yake wa karibu ambaye wakati huo alikuwa mtoto wa rais aliyekuwa madarakani, kuwa Ruto angekuja kuwa Rais wa Kenya baadaye.

Kwa mujibu wa Huddah, aliona dalili za uongozi, uthubutu na maono makubwa kwa Ruto tangu wakati huo, jambo lililomfanya kuwa na imani kubwa na safari yake ya kisiasa hadi kileleni.

Rais William Ruto alichaguliwa kuwa Rais wa tano wa Kenya mwaka 2022, baada ya safari ndefu ya siasa iliyojumuisha changamoto, ushindani mkali na mabadiliko mbalimbali ya kisiasa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *