Msanii wa Bongofleva, Lulu Diva, ametoa onyo kali kwa vijana wa Kitanzania dhidi ya vitendo vinavyoweza kuvuruga amani ya nchi, akiwataka kutoruhusu kushawishiwa au kurubuniwa kuingiza taifa kwenye machafuko.
Kwenye mkao na wanahabari, Lulu Diva ameeleza kuwa amani ni msingi wa maendeleo ya taifa lolote, na pindi inapovunjika, madhara yake huwa makubwa na huchukua muda mrefu kurekebishwa. Kwa mujibu wake, vijana wanapaswa kuwa mstari wa mbele kulinda amani, badala ya kuwa chombo cha kuharibu juhudi za maendeleo ya nchi.
Mrembo huyo, amewataka vijana kuwa makini na ujumbe wanaoupokea hasa kupitia mitandao ya kijamii, akionya kuwa kuna watu wenye maslahi binafsi wanaoweza kuwatumia vibaya. Kwa mtazamo wake, kulinda amani ni jukumu la kila Mtanzania, kwani bila amani hakuna maendeleo wala ustawi wa jamii.
Kauli hiyo imekuja kufuatia hali ya sintofahamu na machafuko yaliyojitokeza nchini Tanzania baada ya uchaguzi, hali iliyosababisha athari kubwa kwa maisha ya wananchi, hususan upande wa uchumi