Rapa kutoka Marekani, Nicki Minaj, ameripotiwa kupoteza mamilioni ya wafuasi kwenye mtandao wa Instagram kufuatia hatua yake ya kuonesha hadharani kumuunga mkono Rais wa Marekani, Donald Trump.
Kwa mujibu wa ripoti mbalimbali, Nicki Minaj hivi karibuni alishiriki katika tukio la kisiasa la Turning Point USA (TPUSA), ambapo alitoa kauli zinazoonekana kumuunga mkono Trump pamoja na mwanaharakati wa kihafidhina, Charlie Kirk.
Ripoti zinaeleza kuwa baada ya tukio hilo, Nicki Minaj alipoteza zaidi ya wafuasi milioni 10 kwenye Instagram ndani ya muda mfupi, kabla ya akaunti yake kutoweka kabisa kwenye jukwaa hilo.
Hadi kufikia Desemba 24, 2025, akaunti rasmi ya Nicki Minaj ya Instagram haionekani tena ila bado anaendelea kuwa active kwenye mtandao wa X (zamani Twitter), ambako ameendelea kushiriki mawazo na kuwasiliana na mashabiki wake.