Msanii mwenye utata nchini Kenya, Akothee, amemshauri hadharani binti yake Rue Baby achague mwanaume mwenye uwezo wa kifedha badala ya kufuata mapenzi pekee katika mahusiano.
Kwa mujibu wa Akothee, uthabiti wa kifedha hujenga msingi imara wa maisha, huku mapenzi yakija baadaye pale mazingira yanapokuwa salama na yenye utulivu.
Mwanamama huyo amesisitiza kuwa atakuwa mwenye furaha zaidi akimuona binti yake Rue Baby akililia Dubai akiwa na tajiri mwenye pesa kuliko alilie kijijini kwao Kanyamkago bila msaada wowote.
Kauli hiyo imezua hisia mseto miongoni mwa watumiaji wa mitandao ya kijamii. Wapo waliounga mkono wakisema ushauri huo unatokana na uzoefu wa maisha na changamoto halisi zinazokumba mahusiano mengi, huku wengine wakipinga wakidai mapenzi ya kweli hayawezi kubadilishwa na maslahi ya kifedha.