Gossip

Vera Sidika Ashangaza Mashabiki, Aonekana Akikama Ng’ombe Kijijini

Vera Sidika Ashangaza Mashabiki, Aonekana Akikama Ng’ombe Kijijini

Socialite kutoka Kenya Vera Sidika amewashangaza mashabiki wake baada ya kushiriki picha zikimuonyesha akifurahia maisha ya kijijini wakati huu wa likizo za Krismasi katika Kaunti ya Kakamega.

Kupitia ukurasa wake wa InstaStory, Vera amechapisha misururu ya picha akionekana akikama ng’ombe, jambo lililozua gumzo kubwa mitandaoni kutokana na wengi kumzoea akiwa anaishi maisha ya kifahari maeneo ya mijini.

Mrembo huyo amembatanisha picha hizo na ujumbe unaosomeka “Shikwekwe, the village baddie has arrived,” akionyesha furaha kuhusu kurejea kwenye asili yake ya kijijini.

Picha hizo zimesambaa kwa kasi mitandaoni huku wengine wakisema ni funzo kwamba maisha ya kijijini nayo yana mvuto na uzuri wake, hata kwa mastaa wakubwa kama Vera Sidika.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *