Msanii na mjasiriamali kutoka Tanzania, Shilole, amepokea rasmi tuzo ya ZIKOMO kupitia kipengele cha Tuzo Bora ya Biashara Ndogo ya Mwaka 2025.
Katika ujumbe wake wa shukrani alioutoa kupitia mitandao ya kijamii, Shilole ameonyesha furaha kubwa na kuwatolea uvivu wakosoaji wake. Amesisitiza kuwa chuki na maneno ya kubeza hayamzuii kufikia malengo yake, bali huona ni aina ya upendo unaompa nguvu ya kuendelea kupambana.
Shilole amewashukuru mashabiki wake kwa sapoti na upendo mkubwa, akisema hajawahi kuchoka kupokea mapenzi yao wala kutoa shukrani zake. Lakini pia, amemshukuru Mungu kwa neema hiyo na kupongeza waandaaji wa tuzo za ZIKOMO kwa kumpa heshima hiyo.
Katika ujumbe wake, Shilole ameeleza kuwa tuzo hiyo ni hatua muhimu kuelekea ndoto yake ya kukuza biashara ndogo kuwa biashara kubwa siku za usoni. Amesisitiza kuwa sapoti ya mashabiki na wadau ndiyo nguzo ya mafanikio yake.