Msanii wa Bongo Fleva, Pipi Jojo, ametoa shukrani zake za dhati kwa mashabiki wote waliomuunga mkono tangu aanze safari yake ya muziki hadi kufikia hatua ya kuachia EP yake I Want to Make My Mama Proud.
Akizungumza akiwa kwenye ziara yake ya kimuziki nchini Uganda, Pipi Jojo amesema upendo na sapoti kutoka kwa mashabiki imekuwa chachu kubwa ya mafanikio yake.
Msanii huyo pia ametumia fursa hiyo kuweka wazi mipango yake mikubwa ya mwaka 2026, akieleza kuwa analenga kufanya kolabo na wasanii wa Uganda kama sehemu ya juhudi za kuupeleka muziki wa Bongo Fleva katika jukwaa la kimataifa.
Pipi Jojo, ambaye kwa sasa yupo chini ya usimamizi wa baba yake Chief Godlove, anaendelea kufanya vizuri kwenye soko la muziki kupitia wimbo wake mpya “With You”, aliowashirikisha Chid Benz na Country Wizzy, wimbo unaoendelea kupata mapokezi makubwa kutoka kwa mashabiki wa muziki wa Afrika Mashariki.