Msanii wa Bongo Fleva Harmonize amewasisimua mashabiki wake baada ya kukiri hadharani kuwa Kajala Masanja ndiye mwanamke mrembo zaidi kuwahi kumuona duniani, kauli aliyotoa akiwa jukwaani pamoja na Kajala huko Zanzibar.
Tukio hilo lilitokea usiku wa kuamkia leo wakati wa burudani, ambapo Harmonize na Kajala walionekana wakishindwa kujizuia hisia zao mbele ya umati wa mashabiki. Baada ya kupigana mabusu yaliyozua shangwe na makelele, Harmonize alimwaga sifa nzito kwa Kajala, akisema uzuri wake hauna kifani na hajawahi kumuona mwanamke mwingine anayemfikia duniani.
Akizungumza mbele ya mashabiki zake, Harmonize amesisitiza kuwa mapenzi yake kwa Kajala hayajawahi kufifia licha ya changamoto zilizowahi kuwakumba. Ameeleza wazi kuwa kamwe hataacha kumpenda Kajala, kauli iliyowagusa wengi na kuzua hisia mseto miongoni mwa waliohudhuria.