Entertainment

Dyana Cods Adokeza Kuja na Bidhaa Maalum Kutangaza Albamu ya Ghetto Girl

Dyana Cods Adokeza Kuja na Bidhaa Maalum Kutangaza Albamu ya Ghetto Girl

Msanii wa muziki kutoka Kenya, Dyana Cods, amedokeza mpango wa kuja na bidhaa maalum (merchandise) kama njia ya kuitangaza albamu yake mpya ya Ghetto Girl, iliyoachiwa rasmi mapema mwezi huu wa Desemba.

Kupitia mitandao ya kijamii, Dyana Cods amewapa ishara mashabiki wake kuwa yuko mbioni kuzindua bidhaa zenye nembo ya Ghetto Girl, hatua inayolenga kuongeza hamasa na kuendeleza ujumbe wa albamu hiyo.

Ingawa T-shirt zinatajwa kuwa miongoni mwa bidhaa zitakazokuwepo, msanii huyo ameacha nafasi kwa mashabiki kupendekeza bidhaa nyingine wanazotamani ziongezwe.

Mpango huo umeonekana kama mkakati wa masoko unaolenga kuimarisha brand ya Ghetto Girl na kuifanya albamu hiyo izidi kuwafikia mashabiki wengi zaidi, huku pia ukitengeneza muunganiko wa karibu kati ya msanii na wafuasi wake.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *