Staa wa muziki nchini Kenya, Willy Paul, ametoa onyo kali kwa wakosoaji wake akiwataka wajiandae kwa kipindi kigumu katika mwaka mpya wa 2026, akisema kuwa atakuwa kila mahali kama hewa ya oksijeni.
Kupitia mitandao yake ya kijamii, Willy Paul amesisitiza kuwa hakuna kitu kitakachomzuia kutimiza malengo yake licha ya chuki, maneno ya kukatisha tamaa na ukosoaji unaomkabili mara kwa mara.
Msanii huyo amesema kuwa ukimya wake katika kipindi cha sikukuu za mwisho wa mwaka 2025 haukuwa dalili ya kupotea, bali ulikuwa ni maandalizi ya kurejea kwa nguvu zaidi.
Hata hivyo ameongeza kuwa mwaka 2026 utakuwa wa kihistoria kwake, akiahidi kutoa kazi nyingi zitakazomuweka kwenye kila kona ya tasnia ya burudani, kuanzia redio, mitandao ya kijamii hadi majukwaa ya muziki.