Gossip

Stevo Simple Boy Amkataa Hadharani Pritty Vishy

Stevo Simple Boy Amkataa Hadharani Pritty Vishy

Msanii wa muziki kutoka Kenya, Stevo Simple Boy, ameibuka na kauli nzito dhidi ya aliyekuwa mpenzi wake Pretty Vishy, akidai kuwa hamtambui kama mtu maarufu nchini humo.

Akizungumza na Mannu Podcast, Stevo amesema Pretty Vishy alitumia kivuli cha mahusiano yao kujitengenezea jina na kujipendekeza kwa umma, akisisitiza kuwa umaarufu wake ulitokana zaidi na kuhusishwa naye kimapenzi kuliko juhudi binafsi.

Stevo pia ameweka wazi kuwa hana mpango wa kurudiana naye, hata kama angepewa nafasi hiyo. Kulingana na msanii huyo, sababu kuu ni tabia mbaya ambazo anadai haziwezi kuvumilika katika uhusiano.

Kauli hiyo imeibua mjadala mkubwa mitandaoni, huku mashabiki wakigawanyika, baadhi wakimuunga mkono Stevo kwa kusema anasema ukweli wake, huku wengine wakimtetea Prity Vishy wakidai kuwa pia amejitahidi kujijengea jina lake kupitia mitandao ya kijamii.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *