LifeStyle

Harmonize Aonyesha Mapenzi ya Dhati kwa Kajala Kupitia Simu Yake

Harmonize Aonyesha Mapenzi ya Dhati kwa Kajala Kupitia Simu Yake

Staa wa muziki kutoka Tanzania, Harmonize, amewapa wanaume darasa la mapenzi kuhusu namna wanavyopaswa kuwa-save wapenzi wao kwenye simu zao.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Harmonize ameposti picha ya screenshot inayoonyesha namna alivyomsave mke wake Kajala Frida kwenye simu yake. Kilichowavutia wengi ni jina alilotumia, ambapo amemsave Kajala kama “I Was Made for Her” kwa maana ya aliumbwa kwa ajili yake.

Hatua hiyo imeibua hisia mseto miongoni mwa mashabiki, wengi wakimpongeza Konde Boy kwa kuonyesha mapenzi ya dhati kwa mpenzi wake Kajala. Wengine wamechukulia kama ujumbe mzito kwa wanaume kuhusu kuthamini na kuheshimu wake zao bila aibu.

Wawili hao wameendelea kudhihirisha kuwa mapenzi yao yamerudi kwenye ubora wake wa juu, kinyume na madai ya baadhi ya watu waliodai kuwa uhusiano wao ni kiki tu kwa ajili ya kutafuta umaarufu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *