Content creator maarufu mtandaoni, Chief Godlove, amefunguka kuwa mwezi wa Januari 2026 pekee tayari umemuingizia mamilioni ya fedha zitakazomwezesha kuendesha maisha yake kwa miaka mitano ijayo bila matatizo yeyote.
Kupitia mitandao yake ya kijamii, Chief Godlove ameonekana kujiamini kupita kiasi kwa kusema kuwa kwake mwaka tayari umeshaisha, ilhali kwa wengine ndio kwanza unaanza.
Mbali na mafanikio ya kifedha, Chief Godlove pia amejitwika mataji mazito, akidai kuwa kwa sasa ndiye kijana mwenye ushawishi mkubwa zaidi barani Afrika, sambamba na kuwa kijana mwenye pesa nyingi kuliko kijana yeyote Afrika.
Chief Godlove hakuishia hapo, ameenda mbali zaidi na kudai kuwa ndiye kijana mwenye akili nyingi zaidi Afrika Mashariki na Kati, akisisitiza kuwa mafanikio yake hayajatokana na bahati bali akili, mipango na maamuzi sahihi.