TikTok ya nchini Marekani sasa inaendeshwa chini ya umiliki na usimamizi mpya, kupitia kampuni iitwayo TikTok USDC, inayosimamia shughuli zote za jukwaa hilo ndani ya Marekani.
Hatua hiyo inakuja baada ya mijadala ya muda mrefu kuhusu usalama wa data za watumiaji, uwazi wa uendeshaji, pamoja na masuala ya ushawishi wa majukwaa ya mitandao ya kijamii. Mabadiliko hayo yameanza kuleta mjadala mpana miongoni mwa watumiaji na watengenezaji wa maudhui.
Wakati huo huo, mabadiliko hayo yameanza kuathiri tabia za watumiaji. Ripoti zinaonesha kuwa baadhi ya creators wameendelea kutumia TikTok kama kawaida, huku wengine wakianza kuhamia au kujaribu majukwaa mbadala kama Instagram Reels na YouTube Shorts, wakilenga usalama na uthabiti wa muda mrefu.
Kwa sasa, TikTok ya Marekani ipo katika kipindi cha mpito, huku wadau wakisubiri kuona utekelezaji wa sera mpya na athari zake kwa watumiaji, creators, na tasnia ya mitandao ya kijamii kwa ujuml