LifeStyle

Bahati aachia diss track kwa Toxic na Buruklyn Boyz kuzima sakata la DNA

Bahati aachia diss track kwa Toxic na Buruklyn Boyz kuzima sakata la DNA

Msanii wa muziki nchini Kenya, Bahati, kwa mara nyingine tena amejikuta kwenye kitovu cha mjadala mtandaoni baada ya kuachia wimbo wake mpya wa “diss” uitwao β€œLost Kwa Throne.”

Katika wimbo huo, Bahati amewatupia dongo la moja kwa moja kundi la Drill la Buruklyn Boyz pamoja na rapa Toxic Lyrikali, akiwashushia mistari mikali inayodai kuwa amerejea kutawala kiti cha enzi cha muziki wa Kenya.

Hata hivyo, kuachiwa kwa wimbo huu kumekuja wakati ambao msanii huyo yuko kwenye shinikizo kubwa la umma kuhusu sakata la DNA. Hivi karibuni, mama mmoja alijitokeza na kudai kuwa ndiye mama mzazi wa Bahati, madai ambayo yalizua taharuki na kumfanya msanii huyo kukubali kufanya vipimo vya kisayansi.

Licha ya Bahati kukubali kufanya vipimo hivyo, amekuwa mzito kuweka wazi matokeo hayo, jambo ambalo limeibua maswali mengi. Inasemekana kuwa Bahati anatumia wimbo huo kugeuza upepo wa mazungumzo mtandaoni (distraction) ili kuwasaulisha watu sakata la DNA linalomkabili.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *