Gossip

Koffi Olomide Achora Tattoo ya Sura ya Mkewe Cindy Le Coeur Kifuani

Mkongwe wa muziki kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Koffi Olomide, amechora tattoo kifuani kwake yenye sura ya mkewe, Cindy Le Coeur.

Kupitia Instastory yake, msanii huyo ameposti picha akionekana akiwa katika hatua ya kuchorwa tattoo hiyo, huku mchoro huo ukionyesha sura ya Cindy ikiwa imechorwa kifuani kwake.

Hatua ya Koffi Olomide kuchora tattoo ya mkewe imekuja siku chache tu baada ya wawili hao kufunga ndoa rasmi, kufuatia uhusiano wao wa kimapenzi uliodumu kwa zaidi ya miaka 20.

Kwa muda mrefu, Cindy Le Coeur amekuwa sehemu muhimu ya maisha na kazi ya Koffi Olomide, akifanya naye kazi kama mmoja wa waimbaji wakuu katika kundi lake la muziki. Mahusiano yao ya muda mrefu hatimaye yalifikia hatua ya ndoa, jambo lililoshangiliwa na mashabiki wengi wa muziki wa Congo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *