Mwanamitandao kutoka Kenya Diana Marua amezima tetesi za kuachana na mume wake Bahati kwa ujumbe mzito wa mahaba
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Diana ameposti video inayowaonyesha wawili hao wakiwa katika hali ya furaha na mahaba, ambapo amekiri kuwa safari yao ya ndoa haijakuwa rahisi kwani wamepitia changamoto nyingi zilizojaribu msingi wa imani na upendo wao
Diana amemsifia mumewe kwa kusimama imara kama mwanamume anayezingatia maagizo ya Mungu katika kulinda familia yake. Ameeleza kuwa kila wanapokutana na vikwazo, Bahati amekuwa akijitolea kwa hali na mali kuhakikisha ndoa yao inasalia thabiti, jambo linalomfanya ajihisi mwenye baraka tele kuwa naye.
Hatua hii imekuja baada ya wawili hao kuonekana kutofuatana (unfollow) kwenye Instagram hivi karibuni, hali iliyowafanya wengi kuhisi kuwa huenda kulikuwa na mgogoro mkubwa.