Mwanamuziki kutoka Kenya King Kaka amesaini rasmi mkataba mpya wa ushirikiano na kampuni kubwa ya muziki Universal Music Group kupitia tawi lake la Universal Music East Africa.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Universal Music East Africa, makubaliano hayo mapya yatawezesha msanii huyo kufanya kazi kwa karibu na kampuni hiyo ya kimataifa huku akiendelea kusimamia kazi zake kupitia lebo yake ya muziki ya Kaka Empire.
Kupitia ushirikiano huo, pande zote mbili zinalenga kupanua usambazaji wa muziki wa Afrika Mashariki katika masoko ya kimataifa na kuwafikia wasikilizaji wengi zaidi duniani.
Hatua hiyo inatajwa kuwa fursa muhimu kwa King Kaka na wasanii wanaofanya kazi chini ya Kaka Empire, kwani itawawezesha kufaidika na mtandao mpana wa usambazaji, masoko na rasilimali za kimataifa za Universal Music Group.