Msanii wa muziki, Bahati, amewataka Wakenya kuacha kumtupia lawama kufuatia mjadala unaoendelea kuhusu matokeo ya vipimo vya DNA vinavyohusiana na madai ya uzazi wake.
Kupitia ujumbe aliouchapisha mtandaoni, Bahati amesema amekuwa akipokea shinikizo kubwa kutoka kwa umma tangu matokeo hayo yalipotangazwa. Ameeleza kuwa baadhi ya watu wamekuwa wakimshutumu kuwa huenda alihonga madaktari ili kubadilisha matokeo ya vipimo hivyo.
Msanii huyo amekanusha madai hayo na kusema kuwa hakuhusika kwa njia yoyote na mchakato wa kitaalamu wa vipimo hivyo. Amesema matokeo ya DNA hutolewa na wataalamu wa maabara kwa misingi ya kisayansi, hivyo si jambo linaloweza kubadilishwa kwa urahisi kama baadhi ya watu wanavyodai.
Bahati pia ameomba apewe faragha ili aweze kukabiliana na hali hiyo kwa utulivu, akisisitiza kuwa mjadala huo umeathiri maisha yake binafsi pamoja na familia yake.