
Staa wa muziki nchini Willy Paul ameamua kumjibu msanii chipukizi aitwaye JR Music Kenya kwa kukosoa uimbaji wake kwenye muziki.
Kupitia ukurasa wake wa Twitter amedai kuwa hajawahi kumlazimisha mtu kusikiliza muziki wake na yeyote ambaye anahisi nyimbo zake hazifurahishi arekodi wimbo wake mwenyewe ambao utamfurahisha.
Hitmaker huyo wa “Tamu Walahi” ametoa matusi ya nguoni kwa msanii huyo kwa kusema kwamba hana muda wa kupishana naye kwa sasa ikizingatiwa kuwa amejikita zaidi kwenye suala la kutoa muziki mzuri.
Kauli ya Willy Paul imekuja mara baada ya msanii JR Music kudai anashangazwa namna Willy paul anashindana na Bahati wakati muziki wao duni huku akionekana kumuunga mkono Mchekeshaji Eric Omondi ambaye amekuwa akiwashinikiza wasanii wa Kenya waache kulaza damu kwenye muziki wao.
Hakuishia hapo alienda mbali zaidi na kuuponda muziki wa msanii Otile Brown kwa kusema kwamba msanii huyo ameishiwa na mawazo kwa sababu katika siku za karibuni amekuwa akilazimisha mistari kwenye nyimbo zake.
Hata hivyo baadhi watumiaji wa mitandao ya kijamii wamemkingia kifua Willy Paul kwa kumshambulia jamaa huyo kwa kusema kuwa atoe muziki mzuri kwanza badala ya kutumia majina ya wasanii hao kujitafutia umaarufu.