Entertainment

Eric Omondi apigwa marufuku kuhudhuria tamasha la Sol Fest 2022

Eric Omondi apigwa marufuku kuhudhuria tamasha la Sol Fest 2022

Ikiwa imesalia siku chache kabla ya tamasha la Sol Fest , Msanii Bien ameweka mkazo juu ya msimamo wa Sauti Sol kutomruhusu mchekeshaji Eric Omondi kuhudhuria tamasha lao linalotarajiwa kufanyika Desemba 17 mwaka huu jijini Nairobi.

Kupitia post yake aliyoiweka Instagram, Bien amewahakikishia mashabiki watakao hudhuria tamasha la Sol Fest kwamba Eric Omondi hatoruhusiwa kamwe kuingia kwenye tamasha hilo.

Bien pia amedai kuna uwezekano mkubwa Eric Omondi akatumia janja janja za kila aina kuzamia kwenye tamasha hilo, lakini hatofanikiwa kutokana na ulinzi madhubuti utakao wekwa.

Video Clip ya hivi karibuni ikimuonyesha Eric Omondi akiongea na waandishi wa habari kuhusu kuchukiwa na wasanii wengi nchini, inasadikika ndio chanzo cha zuio hilo kutoka kwa wana Sauti Sol.

Omondi kwenye mahojiano hayo alidai ana maadui wengi sana hasa wasanii, hivyo kila tamasha atakalo kuwa akihudhuria basi atakuwa na ulinzi mkubwa wa watu na mbwa, akilitolea mfano tamasha la Sol Fest kuwa atahudhuria tamasha hilo akiwa na idadi ya mbwa 20.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *