Entertainment

Eddy Kenzo ajibu madai ya Bebe Cool kuwa amebebwa na bahati kwenye muziki

Eddy Kenzo ajibu madai ya Bebe Cool kuwa amebebwa na bahati kwenye muziki

Nyota wa muziki nchini Uganda Eddy Kenzo amejibu madai ya Bebe Cool kuwa bahati ndio imembeba kwenye muziki.

Kwenye mahojiano yake hivi karibuni Kenzo amesema Bebe Cool anatumia madai hayo kujifariji huku akidai kuwa bidii ndio imempa mafanikio makubwa kwenye muziki wake kwa miaka 10 na sio bahati kama namna ambavyo Bosi huyo wa Gagamel anavyodai.

Hitmaker huyo wa “Nsimbudde” amesema Bebe Cool anapaswa kukubali kuwa ameacha alama kwenye tasnia ya muziki nchini Uganda badala ya kuwahada mashabiki na taarifa za uongo.

“Bebe Cool alisema nina bahati kwa sababu alitaka kujifariji. Huwezi kuwa na bahati milele, najua ninachofanya na nimestahili kile nilichonacho. Anapaswa kukubali na kuwaambia watu wake kwamba Kenzo amefanya muziki kwa zaidi ya miaka 10 na anafahamu hilo,” alisema Eddy Kenzo.

Kauli ya Eddy Kenzo inakuja mara baada ya Bebe Cool kuachia orodha ya wasanii waliofanya vizuri mwaka 2022 ambapo alimtaja Kenzo kama msanii aliyebebwa na bahati kwenye muziki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *