
Meneja wa Harmonize, Dk. Sebastian Ndege maarufu Jembe ni Jembe amefichua kuwa Kajala Msanja sio Meneja tena katika Lebo ya Konde Music Worldwide yake Harmonize.
Hata hivyo, amesema Kajala ameendelea kuwa mwanafamilia na anaamini mahusiano yake na Harmonize hayajawahi kuharibu kazi.
“Yeye ni mpenzi wa zamani wa msanii wangu ila sio sehemu ya Lebo, alikuwa Meneja lakini si Meneja tena kwa sababu mambo yalikuwa yanagongana, uhusiano, kazi, familia.” alisema.
“Tunamheshimu na tunathamini mchango wake kwa Konde Gang na uhusiano aliojenga alipokuwa nasi. Tulifurahi.” alisisitiza Jembe.