
Rapa kutoka nchini Uganda Gravity Omutujju amefufua tena bifu yake na msanii mkongwe Jose Chameleone.
Kwenye mahojiano yake hivi karibuni Omutujju amesema hana mpango kumuunga mkono Chameleone kwenye shoo yake ijayo, itakayofanyika huko Lugogo, Cricket Oval.
Gravity Omutujju amesema shoo ya msanii huyo itabuma vibaya huku akidai kwamba hatokuja kumheshimu Jose Chameleone kwa sababu hajawahi kumfanyia kitu chochote kizuri kwenye maisha yake.
“Siwezi kumuunga mkono, hajawahi kunisaidia kwa namna yoyote ile. Mwache apambane na hali yake, asitarajie msaada kutoka kwangu. Sijali hata kuhusu onesho la Chameleone kwa sababu si mtu mzuri,” alisema.