Entertainment

Bien wa Sauti Sol ahirisha ziara yake ya muziki nchini Marekani

Bien wa Sauti Sol ahirisha ziara yake ya muziki nchini Marekani

Mwimbaji maarufu nchini Kenya anayeunda kundi la Sauti Sol, Bien Aime Baraza ametangaza kuahirisha ziara yake ya muziki nchini Marekani

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Duke Concept Entertainment kupitia ukurasa wao rasmi wa Instagram, maamuzi hayo yametokana na kukosekana kwa baadhi ya wanachama muhimu wa bendi ambao kwa mujibu wao ingeathiri mchakato mzima wa kutoa burudani kwa mashabiki.

Pamoja na kuahirisha ziara hiyo Bien amewaomba radhi mashabiki zake kwa usumbufu uliojitokeza huku akiwajuza walionunua tiketi kuwa wasiwe na hofu kwani tiketi hizo zitatumika pale watakapotangaza tena kufanyika kwa shows hizo hivi karibuni.

Bien alipaswa kuanza ziara yake hiyo ya “Alusa Why Are You Topless” mnamo tarehe 5 mwezi Februari mwaka huu ambapo angeanzia huko Atalanta na kuihitimisha Februari 16 Jijini New York.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *