Gossip

Stevo Simple Boy na Mkewe Brenda Watarajia Mtoto wa Kwanza

Stevo Simple Boy na Mkewe Brenda Watarajia Mtoto wa Kwanza

Msanii wa muziki wa hip hop nchini Kenya, Stevo Simple Boy, amefichua habari njema kuhusu maisha yake ya kifamilia kwa kutangaza kuwa mkewe, Brenda, ni mjamzito wa miezi mitatu.

Stevo alitoa tangazo hilo kwa furaha wakati wa mahojiano maalum na mchekeshaji Tumbili, ambapo alikuwepo pamoja na mkewe Brenda. Akiwa mwenye bashasha, msanii huyo alieleza kuwa wanatarajia mtoto wao wa kwanza, na kuongeza kuwa ni baraka kubwa katika maisha yao.

“Nashukuru Mungu kwa hii baraka. Brenda ni mjamzito wa miezi mitatu sasa, na tunatarajia kila kitu kiende vizuri,” alisema Stevo Simple Boy huku Brenda akitabasamu kwa furaha pembeni yake.

Habari hizo zimepokelewa kwa furaha na mashabiki wa msanii huyo, wengi wakimpongeza na kumtakia mema katika hatua hii mpya ya maisha. Stevo Simple Boy, anayejulikana kwa nyimbo zenye ujumbe wa kijamii kama “Mihadarati” na “Freshi Barida”, ameendelea kuvutia mashabiki si tu kwa muziki wake bali pia kwa unyenyekevu na maadili anayoyaonyesha hadharani.

Mashabiki sasa wanangoja kwa hamu kuona safari yao ya uzazi ikiendelea, huku wengine wakipendekeza majina ya mtoto wao mtarajiwa kwenye mitandao ya kijamii.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *