Entertainment

Mfululizo wa Picha za Drake Mtandaoni Wazua Tetesi za Albamu Mpya Iitwayo Ice Man

Mfululizo wa Picha za Drake Mtandaoni Wazua Tetesi za Albamu Mpya Iitwayo Ice Man

Rapa nyota wa Canada, Drake, amezua gumzo mitandaoni baada ya kuchapisha mfululizo wa picha kwenye ukurasa wake wa Instagram, ambazo mashabiki na wachambuzi wa muziki wanazitafsiri kama uthibitisho wa albamu yake mpya kwa jina la ICEMAN.

Katika chapisho lake kwenye akaunti rasmi ya Instagram (@champagnepapi), Drake alionekana kuweka picha ya mandhari ya theluji yenye mlima uliofunikwa na barafu, na chini yake akaandika kwa herufi kubwa; ICEMAN. Chapisho hilo limepokea zaidi ya likes milioni moja na maelfu ya maoni kutoka kwa mashabiki waliotafsiri ujumbe huo kama tangazo la jina la albamu mpya.

Drizzy pia alichapisha picha za watu mbalimbali mashuhuri wanaohusiana na jina hilo, ikiwa ni pamoja na Bobby Drake, mhusika wa Marvel Comics, Kimi Räikkönen, dereva wa zamani wa Formula 1 na Val Kilmer, ambaye aliigiza kama Iceman katika filamu ya Top Gun.

Hata hivyo, Drake hajatoa tamko rasmi kuthibitisha jina la albamu hiyo, lakini machapisho hayo yameongeza matarajio makubwa miongoni mwa mashabiki wake duniani kote. Albamu hii itakuwa kazi yake ya kwanza ya solo tangu kutolewa kwa For All The Dogs mwaka 2023.

Kwa sasa, wapenzi wa muziki wanasubiri kwa hamu taarifa rasmi kutoka kwa rapa huyo anayejulikana kwa ubunifu wa hali ya juu na mbinu za kipekee za kusisimua kwenye mitandao ya kijamii

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *