Tech news

Instagram Yaboresha DM kwa Kutafsiri Ujumbe wa Sauti na Kuongeza Muda

Instagram Yaboresha DM kwa Kutafsiri Ujumbe wa Sauti na Kuongeza Muda

Kampuni ya Meta imeendelea kuboresha huduma zake kwa watumiaji wa Instagram kwa kutangaza mabadiliko mapya katika sehemu ya ujumbe wa moja kwa moja (DM). Maboresho hayo yanahusisha uwezo wa kutafsiri ujumbe wa sauti kuwa maandishi (voice message transcription), pamoja na kuongeza muda wa ujumbe wa sauti kutoka dakika 1 hadi dakika 5.

Kwa mara ya kwanza, watumiaji wa Instagram sasa wataweza kuona maneno ya ujumbe wa sauti kama maandishi, jambo linalowezesha mawasiliano kuwa rahisi hata pale ambapo mtu hawezi kusikiliza sauti moja kwa moja. Kipengele hiki kinatarajiwa kuwa msaada mkubwa kwa watumiaji walioko katika mazingira ya utulivu au wale wenye changamoto ya kusikia.

Aidha, kwa muda mrefu, ujumbe wa sauti katika DM ulikuwa umewekewa kikomo cha dakika moja tu. Lakini kwa maboresho haya, watumiaji sasa wanaweza kutuma ujumbe wa sauti wa hadi dakika tano, jambo linalowapa uhuru zaidi wa kueleza na kuwasiliana bila kukatizwa.

Mabadiliko haya ni sehemu ya juhudi za Meta kuboresha uzoefu wa watumiaji kwenye majukwaa yake, huku Instagram ikiendelea kushindana na majukwaa mengine ya mawasiliano kama WhatsApp, Telegram, na Signal.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *