
Msanii wa R&B na mfanyabiashara Ray J ameibuka kwa hasira na kumshambulia vikali Suge Knight baada ya madai ya kushangaza aliyoyatoa kwenye kipindi cha televisheni cha Piers Morgan, ambapo Suge alisema kuwa Ray J na Diddy walikuwa na uhusiano wa kimapenzi. Madai haya yamezua hisia kali kwa Ray J na mashabiki wake.
Ray J, ambaye awali alikuwa akimheshimu Rais huyo wa zamani wa Death Row Records, na kumtetea, alisema amevunjika moyo na kauli hizo zisizo na msingi. Alidai kuwa Suge amemshambulia kwa njia chafu na kuonyesha tabia ya kutojali, licha ya kuwa amekuwa akimuunga mkono katika nyakati ngumu.
Aidha, Ray J alilalamikia namna Suge alivyoikosea heshima brand yake ya The Gaygency, inayosaidia wasanii wa jamii ya LGBTQIA+. Alisisitiza kuwa kuunga mkono jamii hiyo hakumaanishi kuwa yeye binafsi ni mpenzi wa jinsia moja, na ni aibu kwa Suge kutumia hilo kumshambulia.
Ray J pia alimtuhumu Suge kuwa mtu anayeudhulumu watu wa karibu, ikiwemo wanaume na wanawake. Hadi sasa, Suge hajajibu madai hayo, huku mjadala ukiendelea kuenea mitandaoni kwa hisia kali kutoka kwa wafuasi wa pande zote.