
Hatimaye ahadi ya Harmonize ya kuingia studio na kufanya kolabo na 20 percent pindi tu akitua Tanzania kutoka nchini Marekani imepokelewa kwa mikono miwili na mkali huyo wa zamani.
20 Percent ametumia insta story yake kwenye mtandao wa Instagram kumjibu Harmonize kuwa “Promise is like a debt” kwa maana yupo tayari hivyo Harmonize atimize alichokiahidi.
20 percent ambaye ni mshindi wa tuzo tano za Kili Music Awards mwaka wa 2010, aliwahi kutamba na ngoma kama Maisha ya Bongo, Mama Neema, Money Money, Tamaa Mbaya na nyingine kibao.
Haya yanajiri baada ya usiku wa kuamkia Oktoba 25 kuwa mrefu sana kwa harmonize ambaye alionekana akiburudika na midundo ya 20 Percent na kupelekea kutoa ahadi ya kufanya nae kolabo, sambamba na kueleza kuwa ni ndoto yake ya muda mrefu.