Gossip

Dufla Amvamia Mulamwah Kwa Maneno Makali Mtandaoni

Dufla Amvamia Mulamwah Kwa Maneno Makali Mtandaoni

Msanii wa muziki wa dancehall nchini Kenya, Dufla Diligon, amemkemea hadharani mchekeshaji maarufu Mulamwah, akimtuhumu kwa vitisho na usumbufu wa simu.

Kupitia ujumbe mkali aliouweka katika ukurasa wake wa mitandao ya kijamii, Dufla alieleza hasira zake na kuonyesha kutoridhishwa na tabia ya Mulamwah.

“Mulamwah stop threatening me!! Mimi mahali nimezaliwa wewe hata hauwezi survive. Hizi vitisho punguza… ama unaona mimi sina sauti, I mean I don’t have bass?!! On a serious note, stop calling me na kunitishia, mimi ni warrior, am not a coward!!!!” Dufla aliandika Instagram.

Ujumbe huo umeibua gumzo mitandaoni, huku mashabiki wa muziki na wafuasi wa burudani wakitaka kufahamu chanzo cha mvutano huo. Wengi wameunga mkono msimamo wa Dufla, wakisema kuwa watu maarufu wanapaswa kutumia ushawishi wao kwa njia ya kujenga, si ya kuharibu.

 Siku chache kabla ya taarifa hiyo, Dufla alikuwa amedai kwamba Mulamwah alimblock kwenye Instagram bila sababu ya msingi. Katika ujumbe huo, Dufla alimshauri Mulamwah kuacha kuwa na “feelings” kupita kiasi na kuzingatia mambo ya maana.

Mvutano kati ya wawili hao ulianza miaka michache iliyopita, kufuatia madai kuwa Dufla alikuwa anamnyemelea baby mama wa Mulamwah, Carol Sonnie, jambo ambalo lilizua taharuki kubwa kwenye mitandao ya kijamii wakati huo. Ingawa hakuna uthibitisho wa moja kwa moja kuhusu uhusiano kati ya Dufla na Sonnie, hali hiyo ilisababisha sintofahamu kubwa kati yao.