Gossip

Bien Ajitetea Baada ya Kauli Tatanishi Kuhusu Wanawake wa Kenya

Bien Ajitetea Baada ya Kauli Tatanishi Kuhusu Wanawake wa Kenya

Mwanamuziki maarufu kutoka Kenya na mshiriki wa kundi la Sauti Sol, Bien-Aimé Baraza, amevunja ukimya kufuatia mjadala ulioibuka mitandaoni kuhusu mstari wa wimbo wake mpya unaozungumzia wanawake wa Kenya kuwa na foreheads kubwa (paji kubwa za uso).

Kupitia mtandao wa kijamii wa Instagram, Bien alisisitiza kuwa wimbo wake ni kazi ya sanaa inayopaswa kuchukuliwa kwa upana na si kwa hisia binafsi

Bien aliongeza kuwa kauli yake haikuwa ya matusi bali ya mapenzi na shukrani kwa wanawake wa Kiafrika, hasa mke wake, Chiki Kuruka, ambaye ni mhamasishaji wa mazoezi ya mwili na mpenda sanaa.

 “I love our women with foreheads. I could never be with a woman who doesn’t have a forehead. Have you seen my wife?” Aliandika akimjibu shabiki aliyemkosoa vikali kuhusu wimbo wake mpya unaotajwa kuwa na mistari ya kuudhi, hasa kwa wanawake wa Kenya..

Kauli yake imeibua maoni mbalimbali mitandaoni. Wapo waliomsifu kwa kuwa na ujasiri wa kusimama na kazi yake, huku wakiona mstari huo kama ucheshi wa kawaida, lakini pia wapo waliodai kuwa wasanii wanapaswa kuwa makini zaidi na lugha wanayotumia kwa kuwa wana ushawishi mkubwa kwa jamii.

Bien wa Sauti Sol na Diamond Platnumz wameachia wimbo mpya unaoitwa “Katam”. Wimbo huu umetoka hivi karibuni na umepokelewa vizuri sana na mashabiki wao. “Katam” ni wimbo wa mapenzi unaosherehekea uzuri na umoja barani Afrika, na unawaunganisha wasanii hawa wawili wakubwa wa Afrika Mashariki.