
Kampuni mama ya WhatsApp, Meta, imetangaza kushusha rasmi kiwango cha chini cha mfumo wa simu unaohitajika ili kuendelea kutumia huduma ya WhatsApp.
Kwa sasa, watumiaji wa programu hiyo wanapaswa kuwa na simu zilizo na Android 5 au zaidi, au iOS 15.1 na kuendelea. Simu zinazotumia matoleo ya zamani ya mifumo hiyo ya uendeshaji hazitaweza tena kufikia WhatsApp kuanzia mwezi huu.
Hatua hii inalenga kuboresha usalama na utendaji wa programu hiyo, lakini pia inaathiri maelfu ya watumiaji wa simu kongwe. Kwa upande wa iPhone, simu zinazotumia iOS 12.5.6, kama vile iPhone 5s na iPhone 6, zimeanza kuzuiliwa kutumia WhatsApp.
Watumiaji wa simu hizo watalazimika kubadilisha simu na kutumia vifaa vinavyowezesha kusasisha hadi mifumo ya kisasa ili kuendelea kuwasiliana kupitia WhatsApp.
Meta imeshauri watumiaji kukagua toleo la mfumo wa simu zao kupitia sehemu ya Settings > About Phone au Settings > General > About, na kusasisha mara moja iwapo inawezekana.