
Msanii nyota wa muziki wa Bongo Fleva, Nandy, amepatwa na kigugumizi kuzungumzia taarifa zilizogonga vichwa vya habari kwamba msanii wake wa zamani Yammi alifikiria kujiua kutokana na msongo wa mawazo.
Katika mahojiano maalum na waandishi wa habari, Nandy amesema kuwa taarifa hizo zilimshtua na kumgusa sana, na kwamba anatamani kukutana na Yammi uso kwa uso ili wazungumze kwa kina, badala ya kuwasiliana kwa njia ya simu pekee.
Hata hivyo, Nandy ametumia fursa hiyo kuwaomba waandishi wa habari kuacha kumuliza maswali kuhusu Yammi kila mara anapofanya mahojiano. Amesema hatua hiyo imekuwa ikimletea usumbufu wa kihisia na kuonekana kama chanzo cha matatizo ya hitmaker huyo wa ngoma ya “Raha”.
Tamko hilo la Nandy limekuja wakati mashabiki wengi wakiendelea kutoa maoni tofauti kuhusu uhusiano wa wawili hao, huku baadhi wakihusisha tofauti zao na suala la Yammi kuwa msanii aliyekuwa chini ya lebo ya The African Princess inayomilikiwa na Nandy kabla ya kuondoka kimyakimya