Gossip

Spice Diana Amshambulia Sheebah, Adai Analipa Wanablogu Kumchafua

Spice Diana Amshambulia Sheebah, Adai Analipa Wanablogu Kumchafua

Msanii nyota wa muziki nchini Uganda, Spice Diana, ameendeleza mashambulizi ya maneno dhidi ya msanii mwenzake Sheebah Karungi, akimtuhumu kuwalipa wanablogu na baadhi ya watu kutoka kwenye timu yake ili kusambaza taarifa za kumchafua mtandaoni.

Akizungumza katika mahojiano na kituo cha runinga nchini Uganda, Spice Diana alisema kuwa Sheebah mara nyingi hujikita kumzungumzia kila anapopata nafasi, jambo ambalo kwa upande wake anadai halimsumbui.

Spice Diana amesema kuwa hatua ya kum-unfollow Sheebah kwenye Instagram ilitokana na kile alichokiona kama tabia za kimaslahi binafsi na zisizo za ukweli. Alieleza kuwa badala ya kushughulikia masuala yao binafsi kwa njia ya moja kwa moja, Sheebah alichagua kuchapisha ujumbe kwenye mitandao ya kijamii, hali iliyomfanya apoteze imani naye.

Kwa upande wake, Sheebah Karungi, kupitia mkutano na wanahabari uliofanyika wiki iliyopita, alikanusha madai ya kumshambulia Spice Diana au kulipa wanablogu waandike habari mbaya kumhusu, akieleza kuwa hana sababu yoyote ya kufanya hivyo.

Mvutano kati ya wasanii hawa wawili umeendelea kushika kasi kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii, huku mashabiki wakifuatilia kwa karibu maendeleo ya mzozo huo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *