Gossip

Amber Ray Azua Tetesi za Kutengana na Rapudo, Mashabiki Wadai Amerudi kwa Jimal

Amber Ray Azua Tetesi za Kutengana na Rapudo, Mashabiki Wadai Amerudi kwa Jimal

Sosholaiti maarufu mtandaoni Amber Ray amerudi tena kwenye vichwa vya habari kufuatia tetesi kuwa uhusiano wake na baba wa mtoto wake, Kennedy Rapudo almaarufu Baba Atana, umefika kikomo.

Mashabiki wamedai kumuona Amber akiuza baadhi ya vitu vya nyumbani vinavyohusishwa na Rapudo, jambo lililoibua maswali mengi. Hii inajiri siku chache tu baada ya Rapudo kusema kwamba wao wawili wameamua kuweka mambo yao ya kifamilia mbali na macho ya umma.

Tetesi zaidi zimeibuka kuwa huenda Amber amerejea kwa mpenzi wake wa zamani, mfanyabiashara Jimal Roho Safi. Baadhi ya mashabiki wamedai kuwa ameanza kuashiria uwepo wa uhusiano mpya kati yake na Jimal kupitia mitandaoni.

Uhusiano kati ya Amber Ray na Rapudo umekuwa wa kuvutia macho ya umma, mara kwa mara wakitajwa kwa misukosuko ya kuachana na kurudiana.Tukio hili jipya limegawanya maoni mtandaoni, wengine wakiamini kuwa Amber anaendelea na maisha yake, huku wengine wakitaja tetesi hizo kama kiki ya kimakusudi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *