Entertainment

Harmonize Atamba na Albamu Mpya, Asema Haitaji Tena Kutafutwa

Harmonize Atamba na Albamu Mpya, Asema Haitaji Tena Kutafutwa

Mwanamuziki Harmonize ameibua tafsiri ya kichokozi kwa wapinzani wake baada ya kujitapa kuwa albamu yake ya 31 ikitoka itakuwa kubwa kiasi cha kumtambulisha kwa kila mtu bila shaka.

Kupitia Insta Story yake, msanii huyo alionekana kujiamini kupita kiasi akisema albamu hiyo ni ya kipekee na itakuwa na nguvu ya kumweka kwenye ramani ya muziki kwa namna ambayo hakutakuwa na haja ya kutumia mtandao wa google ili kumjua. Kauli hiyo imefafsiriwa na baadhi ya mashabiki kama dongo kwa wasanii wanaotegemea kiki na mbinu za kibiashara ili kujulikana.

Hata hivyo, msisitizo wake kuhusu albamu hii mpya umeibua maswali iwapo anajaribu kuwapiga vijembe wapinzani wake ndani ya Bongo Fleva hasa bosi wake wa zamani Diamond ambaye anadaiwa kuwa kwenye ugomvi na msanii wake wa zamani Mbosso kutokana uandishi wa wimbo uitwao Pawa.

Mashabiki wake sasa wanangoja kwa hamu ujio wa albamu hiyo kuona kama kweli itatimiza maneno yake au ni tambo za kawaida za kimastaa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *