Tech news

Samsung Kubadilisha Mtindo wa Watermark Katika Picha za Kamera

Samsung Kubadilisha Mtindo wa Watermark Katika Picha za Kamera

Samsung imepanga kuleta mabadiliko makubwa katika namna watermark (alama ya utambulisho) huonekana kwenye picha zinazopigwa kwa simu zake. Hii ni mara ya kwanza kwa kampuni hiyo kufanya mabadiliko makubwa ya style ya watermark tangu kutolewa kwa toleo la One UI 5.0.

Kwa mujibu wa taarifa zilizovuja, mfumo mpya wa One UI 8.5 unakuja na style mpya ya watermark ambayo ni ya kina zaidi na ya kipekee ikilinganishwa na ile ya sasa. Tofauti na watermark ya awali ambayo ilikuwa rahisi na yenye maelezo machache, watermark mpya itaonyesha taarifa nyingi zaidi kuhusu picha husika.

Katika style hii mpya, watermark itaonekana upande wa kushoto chini ya picha, huku upande wa kulia ukiwa na maelezo ya kiufundi kama aina ya lensi, ISO, focal length, exposure value, aperture, shutter speed, pamoja na tarehe na muda halisi ambao picha imepigwa. 

Mabadiliko haya yanachukuliwa kama jitihada za Samsung kuboresha utambulisho wa picha na kuwapa wapiga picha taarifa zaidi kwa ajili ya kumbukumbu au matumizi ya kitaalamu.

Hata hivyo, baadhi ya watumiaji mtandaoni wameanza kutoa maoni wakidai kuwa style hii mpya inafanana sana na ile ya makampuni kama Vivo na Xiaomi, ambayo tayari yanaweka watermark zenye maelezo ya kina kama hayo katika picha zao.

Licha ya ukosoaji huo, mashabiki wa Samsung wanasubiri kwa hamu kuona jinsi mfumo mpya wa One UI 8.5 utakavyoboresha uzoefu wa matumizi ya kamera kwenye simu hizo, hasa kwa wapiga picha wanaopenda maelezo ya kiufundi moja kwa moja kwenye picha zao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *